Storm FM
Storm FM
11 April 2025, 11:32 am

Watoto 102 wa kituo cha kulea watoto yatima cha moyo wa huruma kilicho chini ya kanisa katoliki geita wamekabidhiwa bima za afya za NHIF jana April 09 2025.
Na: Daniel Magwina:
Akizungumza katika zoezi hilo la kukabidhi bima hizo mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema bima hizo zitakwenda kuwasaidia watoto hao kwaajili ya matibabu huku akiwaomba wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia watoto wasiojiweza.
Naye meneja wa NHIF mkoa wa Geita Elias Odhiambo amesema bima hizo ni za mwaka mmoja na kwamba watoto hao watapata huduma kuanzia ngazi ya awali mpaka huduma za kibingwa

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho cha moyo wa huruma Sister Maria Lauda amesema bima hizo zitawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa watoto hao.
Bima za afya kwa watoto yatima ni ngao muhimu inayowahakikishia huduma bora za afya bila mzigo wa gharama kubwa.
Pia Bima inawezesha kupata matibabu kwa wakati, kuzuia magonjwa sugu, na kuboresha afya yao kwa ujumla.Pia bima inasaidia kupunguza changamoto kwa walezi wa vituo vyao, kuwapa nafasi ya kuzingatia malezi na elimu.
