

6 March 2025, 12:05 pm
BAKWATA mkoa wa Geita kupitia mradi wa TABASAMU KWA WOTE waanzisha kituo cha ushonaji na ujasiriamali ili kusaidia vijana wa kike.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Kutokana na kuwepo kwa wimbi la vijana wa kike wanaomaliza elimu ya msingi na sekodari katika eneo la Masumbwe wilayani Mbogwe kukimbilia maeneo ya machimboni na kuanza kutumikishwa katika umri mdogo, baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Geita kupitia mradi wa TABASAMU KWA WOTE wameanzisha kituo cha ushonaji na ujasiriamali ili kuwasaidia vijana hao kujiajili.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho Shekhe mkuu wa wilaya ya Mbogwe Musa Fadhili amesema mradi huo umelenga kuwanusuru vijana hao kwani wengine wanaamua kufanya matendo ya kudhalilisha utu wao kwasababu ya fedha ndogo ya kujikimu.
Baadhi ya wazazi waliokuwepo kwenye uzinduzi wa kituo hicho wamesema watoto wakike wanapohitimu darasa la saba na shule ya sekondari bila kufaulu wanawaza kuolewa katika umri mdogo huku wakiamini mradi huo utakuwa mkombozi kwa watoto wao.
Mkurugenzi wa mradi wa TABASAMU KWA WOTE Sharifu Chinguile amesema mradi huo umelenga kuisaidia serikali kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana wengi kwa sasa inchini.