Pikipiki yalipuka nakuwaka moto mjini Geita
5 April 2021, 12:36 pm
Wakazi wa Mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu mjini Geita wametakiwa kuwa na vifaa vidogo vya kuzimia moto wa awali katika Makazi yao na Sehemu za biashara ili kukabiliana na majanga ya moto yanayoweza kujitokeza katika maeneo yao.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Uwanja Bw Enos Chelehani Kufuatia tukio la Pikipiki kulipuka nakuwaka moto wakati ikifanyiwa matengenezo Mtaani humo.
Kwa upande wake Didas Joseph aliefanikiwa kuuzima moto huo kwa kutumia fire extigisha baada ya jitihada za wananchi kuuzima moto huo kwa kutumia mchanga kugonga mwamba, amesema nivyema wananchi wakatambua umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika sehemu zao za biashara ili kuepuka madhara.
Nao baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo yao ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.