Mfumo wa uchukuaji taka ni kero kwa wakazi.
3 August 2021, 1:33 pm
Na Zubeda Handrish:
Wakazi wa mtaa wa Nyerere Road katika halmashauri ya mji wa Geita, wameuomba uongozi wa serikali ya mtaa huo kusimamia suala la uchukuaji wa taka katika makazi yao kwakua magari yanayobeba taka hizo hupita barabara kuu pekee na kuzisahau baadhi ya barabara za mitaa.
Wameyasema hayo walipozungumza na Storm FM na kuongeza kuwa mara zote magari ya taka hupita barabara kuu na taka nyingi kusalia katika makazi ya watu kwakuwa magari hayo hayapiti mitaani, hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na taka hizo kutelekezwa kwenya kamazi ya watu
Nae muhudumu wa afya mtaani hapo Bi. Chiku Msham amesema kutokana na kutelekezwa kwa taka hizo wananchi wa mtaa huo wapo hatarini kupata magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira hivyo kuna haja ya serikali ya mtaa kutataua changamoto hiyo.
Nae Mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Dua Issa Kaburi amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na kusema ameshalifikisha sehemu husika na kwamba anasubiri utekelezaji hivyo wawe na subira na wavumilivu wakati suluhu ya changamoto hiyo ikitafutwa.