Storm FM

Maajabu ya simu ya ZTE Blade A34 kutoka Tigo

27 July 2024, 11:57 am

Meneja wa Tigo mkoa wa Geita Willington Byekwaso akiwa katika studio za Storm FM. Picha na Ester Mabula.

Kampuni ya mawasiliano nchini Tigo imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuwafikia watanzania zaidi ya milioni 20 ambao wanaendelea kunufaika na huduma zao.

Na: Ester Mabula – Geita

Meneja wa Tigo mkoa wa Geita Willington Byekwaso amesema Tigo imeendelea kutoa ofa mbalimbali kwa wateja wao kupitia huduma zao, ambapo kwa sasa wamekuja na simu mpya iitwayo ZTE BLADE A34 ambao ina uwezo mkubwa wa kupiga picha yenye 4G ambayo imeenea kote nchini

Amesema hayo alipokuwa katika kipindi cha Storm Asubuhi Julai 26, 2024 kupitia studio za Storm FM na kutoa rai kwa wateja kununua simu hiyo kwani ina fursa rafiki ya kulipia kwa kidogo kidogo au kwa kulipa kwa mkupuo

Sauti ya meneja

Mbali na hilo ameeleza kuwa wamejipanga kutembelea katika vijiji na mitaa mbalimbali ya mkoa wa Geita kwaajili ya kuzindua minara yao itakayorahisisha huduma za mawasiliano.

Sauti ya meneja
Isabela Mmbuji mtoa huduma wa Tigo mkoa wa Geita akiwa katika studio za Storm FM. Picha na Ester Mabula

Isabela Mmbuji ni mtoa huduma kutoka Tigo ambaye amesema kwa sasa wanaendelea kutoa ofa mbalimbali kupitia kampeni ya Sako kwa bako ambayo inamaanisha kuwa pamoja na wateja wao

Sauti ya mtoa huduma