UVCCM Geita yaahidi kusimamia fedha za 10%
22 April 2024, 5:58 pm
Baada ya Serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI kutangaza kurejesha mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, UVCCM mkoa wa Geita yaagiza Halmashauri za Geita kutenda haki kwenye utoaji wa mikopo hiyo.
Na Kale Chongela – Geita
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM mkoa wa Geita Ndg. Manjale Magambo ameagiza halmashauri zote za mkoa wa Geita kusimamia vyema fedha za asilimia 10 ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ili ziwafikie walegwa.
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM mkoa wa Geita zilizopo mtaa wa Magogo ambapo amesema baada ya kusitishwa kwa muda hatimaye serikali imerejesha fedha hizo na mgawanyo wake ukiwa ni asilimia 4 kwa vijana, asilimia 4 kwa wanawake na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu.
Aidha ameongeza kuwa ufatiliaji wa fedha hizo utaenda sambamba na ufatiliaji wa vikundi vyote vya halmashauri za mkoa wa Geita ili kuondoa changamoto ya uwepo wa vikundi hewa ambavyo vinarudisha nyuma malengo ya serikali
Kwa upande wao baaadhi ya vijana akiwemo katibu wa wamesema ili vijana waweze kujikwamu kiuchumi kuna haja ya kila kijana kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo na kwamba ni vyema ikatumika kwa matumizi yaliyo sahihi na kwa matumizi mengine tofauti .