Wananchi Geita wajivunia barabara za mitaa
5 April 2021, 6:24 pm
Wananchi mjini Geita wameelezea namna walivyoguswa na kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na watakavyoendelea kumuenzi kwa yale aliyowaachia ikiwamo barabara za mitaa zilizojengwa katika kipindi chake.
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Katundu, Miti mirefu na Nendeni na Aman mjini Geita wamesema wataendelea kumkumbuka kwa mengi huhusani suala la ujenzi wa barabara za mitaani zilizosaidia kunyanyua kwa kiasi kikubwa vipato vyao kutokana na barabara hizo kuwa karibu na maeneo yao ya biashara.
Miongoni mwa mafundi walioshiriki katika ujenzi wa moja ya barabara mjini Geita Zacharia Frank Marwa amezungumza umuhimu wa barabara hizo za mitaa na kuwasihi wana Geita kutunza barabara hizo ili kumuenzi hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika hatua nyingine mwenye kiti wa mtaa wa Katundu Kivukoni Gideon Ally amesema fursa ya barabara hizi kupita katika mtaa wake itaendelea kuwanufaisha wananchi kwa kurahisisha shughuli za usafirishaji na biashara katika kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli