Storm FM

Wakazi wa Ilungwe kuanza ujenzi wa shule ya msingi

1 April 2026, 17:59

Wananchi wa mtaa wa Ilungwe kata ya Nyankumbu wakiwa katika mkutano wa hadhara. Picha na Ester Mabula

“Ujenzi wa shule hii utasaidia watoto wetu kuepuka ajali na kuwasaidia kutembea umbali mfupi kwani maendeleo yoyote hapa duniani ni lazima yaanze na elimu” – Mwenyekiti wa mtaa

Na: Ester Mabula

Ikiwa ni takribani miezi miwili tangu wananchi washiriki zoezi la kusafisha eneo kwaajili ya ujenzi wa shule katika mtaa wa Ilungwe uliopo kata ya Nyankumbu wilayani na mkoani Geita, hatimaye wakubaliana hatua mpya ya kuanza ujenzi.

Mtaa huo unaokadiriwa kuwa na kaya ya 255 zenye watu zaidi ya 2000, wamekubaliana kuchangia shilingi elfu 20 kila kaya kwaajili ya kuanza ujenzi wa shule ya msingi katika eneo hilo ambapo baadhi ya wananchi Ester Madeni na Majaliwa Samwel wameeleza kukubali hatua hiyo.

Sauti ya wananchi

Mwenyekiti wa mtaa huo Daudi Mwanzalima amesema matarajio yao ni kuanza ujenzi mapema mwezi  Mei mwaka huu na kutoa rai kwa wananchi kushiriki kikamilifu ili kufia lengo lililokususdiwa.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa Daudi Mwanzalima
Diwani wa kata ya Nyankumbu Paschal Sukambi, mgeni rasmi akizungumza na wananchi (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Akizungumza mgeni rasmi katika mkutano huo, Diwani wa kata hiyo Paschal Sukambi amesisitiza wananchi kushiriki katika jambo hilo ili kuweza kunusuru wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda maeneo jirani kupata elimu.

Sauti ya Diwani wa kata ya Nyankumbu Paschal Sukambi
Hatua za awali zilizofanyika za kusafisha eneo la kujenga shule katika mtaa huo Picha na Mrisho Sadick