Storm FM
Storm FM
1 April 2026, 17:48

Kwa wilaya ya Geita ongezeko la bei ya mafuta ya petroli limepanda kwa shilingi 956 kutoka bei elekezi ya mwezi Marchi uliopita.
Na: Ester Mabula
Maafisa usafirishaji kutoka halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita wameeleza ugumu wa kutekeleza majukumu yao kwa sasa kutokana na bei ya mafuta kupanda hali ambayo itawalazimu kupandisha bei ya nauli kwa abiria wanaotumia vyombo hivyo vya usafiri.
Ikumbukwe kila Jumatano ya kwanza ya kila mwezi mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) hutangaza bei kikomo za mafuta.

Afisa huduma kwa wateja katika Ofisi za Baraza la ushauri la watumiaji wa Nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Geita Bw. Wadi Omary amesema kupanda kwa bei si Geita pekee bali ni jambo la kitaifa huku akiwahakikishia wakazi wa Geita kuwa mafuta yapo ya kutosha.
Bei elekezi za mafuta kwa wilaya za mkoa wa Geita ni kama ifuatavyo:
Wilaya ya Geita Petroli ni 4,020 na Dizeli ni 4,006 kwa lita moja.
Wilaya ya Bukombe Petroli ni 4,009 na Dizeli ni 3,995 kwa lita moja.
Wilaya ya Chato Petroli ni 4,041 na Dizeli ni 4,027 kwa lita moja.
Wilaya ya Mbogwe Petroli ni 4,058 na Dizeli ni 4,044 kwa lita moja.
Wilaya ya Nyang’hwale Petrol ni 4,035 na Dizeli ni 4,021 kwa lita moja.