Storm FM
Storm FM
01/04/2026, 10:38

Kwa wilaya ya Geita bei ya Petroli kwa lita moja imeongeza kwa shilingi 956 kutoka bei ya mwezi uliopita.
Na: Ester Mabula
Taarifa iliyotolewa Jumatano ya Aprili 01, 2026 na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) imeainisha bei elekezi za mafuta kwa kila mkoa hapa nchini ambazo zitatumika kwa mwezi huu wa nne (April).
Wilaya ya Geita Petroli ni 4,020 na Dizeli ni 4,006 kwa lita moja.
Wilaya ya Bukombe Petroli ni 4,009 na Dizeli ni 3,995 kwa lita moja.
Wilaya ya Chato Petroli ni 4,041 na Dizeli ni 4,027 kwa lita moja.
Wilaya ya Mbogwe Petroli ni 4,058 na Dizeli ni 4,044 kwa lita moja.
Wilaya ya Nyang’hwale Petrol ni 4,035 na Dizeli ni 4,021 kwa lita moja.
Utofauti wa bei hizo na bei za mwezi uliopita wa Marchi ni kama ifuatavyo:
Geita Petroli ilikuwa 3,064 na Dizeli 3,059 kwa lita moja.
Bukombe Petroli ilikuwa 3,053 na Dizeli 3048 kwa lita moja.
Chato Petroli ilikuwa 3,085 na Dizeli 3,080 kwa lita moja.
Mbogwe Petroli ilikuwa 3,102 na Dizeli 3,097 kwa lita moja.
Nyang’hwale Petroli ilikuwa 3,079na Dizeli 3,074 kwa lita moja.