Storm FM
Storm FM
28/03/2026, 13:12

Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta huduma za afya vijiji jirani hatimae wakazi wa Shibalanga wafutwa machozi.
Na Mrisho Sadick – Geita
Wakazi wa Kijiji cha Shibalanga wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wameipongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kuwajengea zahanati, hatua itakayosaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya vijiji jirani.
Wakizungumza baada ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Nyang’hwale kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, wakazi hao wameeleza matumaini yao kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo kutamaliza kabisa changamoto za kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Abdul Mihayo amesema unatekelezwa kwa ufadhili wa TASAF kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, nakwamba upo katika hatua za ukamilishaji huku ukitarajiwa kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo pamoja na vijiji jirani.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya kijamii inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyang’hwale pamoja na wajumbe wake Alhaji Adam Mtore amerishwa na utekelezaji wa mradi huo huku akiwataka wahusika kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili uanze kutoa huduma kwa wananchi haraka kwakuwa siku za nyuma wamepitia katika kipindi kigumu.