Storm FM
Storm FM
14/03/2026, 22:30

“Tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani jumla ya miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bilioni 14 imetekelezwa na TAKUKURU” – Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Crispin Chalamila
Na: Ester Mabula
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeridhishwa na ujenzi wa mradi wa jengo la Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika Wilaya ya Nyang’hwale, mkoani Geita.
Akizungumza leo Marchi 14, 2026 mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt. Damas Ndumbaro mara baada ya kukagua mradi huo, amesema kamati hiyo imejiridhisha na ubora wa mradi pamoja na matumizi sahihi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 386 zilizotumika kukamilisha ujenzi kamili wa mradi huo ambapo amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mh. Ridhiwani Kikwete, kusimamia taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kujifunza kutoka TAKUKURU kuhusu namna bora ya utekelezaji wa miradi.

Akizungumza Waziri Ridhiwani Kikwete amesema utekelezaji wa mradi huo ulizingatia kikamilifu taratibu na miongozo ya ununuzi wa umma, jambo lililochangia ukamilifu wa mradi huo kwa ufanisi.

Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila akieleza tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya sita jumla ya miradi 45 yenye thamani ya shilingi billion 14 imetekelezwa na TAKUKURU.
