Storm FM
Storm FM
05/03/2026, 18:30

GGML Mentorship program ilianzishwa mwaka 2020 ikiwa na lengo la kumsaidia msichana kutimiza ndoto zake kitaaluma sambamba na kumjengea uwezo wa kujiamini.
Na: Ester Mabula
Jumla ya shule sita za sekondari ambazo ni Nyalwanzaja, Kamena, Kasota, Bugando, Bugurula na Butundwe zimefikiwa na mpango wa GGML Mentorship program ambao unalenga kutoa elimu ya utambuzi kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mpango huo wa kutoa elimu mafunzo na kuwajengea wasichana uwezo wa kujiamini ulianzishwa mwaka 2020 ambao umetajwa kuwa chachu ya kuongeza ufaulu kwa wasichana kama wanavyobainisha Lilian Hamis mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Bugurula na Doris Alfred mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Butundwe.

Wakuu wa shule za sekondari Butundwe na Bugurula Mwl. Happines Manyama na Embola Palangyo wanaeleza kuwa mpango huo umekuwa na tija kitaaluma kwa watoto wa kike sambamba na kuchochea ari ya kupenda masomo ya sayansi.
Akielezea dhamira ya kuanzisha mpango huo Msimamizi wa Rasilimali watu kutoka GGML Khadija Kisatu amesema, mpango huo unasimamiwa na wafanyakazi wanawake wa GGM ambapo ulianzishwa baada ya kubaini kuwa wasichana wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali vinavyopelekea kukwamisha ndoto zao.
