Storm FM

Wakazi Nyantorotoro B walia miundombinu duni msimu wa mvua

26/02/2026, 15:47

Sehemu ya ardhi ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha na Ester Mabula

Licha ya mvua kuleta neema kwa wakulima , hali imekuwa tofauti kwa wakazi wa Nyatorotoro B, kata ya Nyankumbu wilayani na mkoani Geita kwani wanalazimika kulala wakiwa wamesimama.

Na: Ester Mabula

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini, Wakazi wa mtaa wa Nyantorotoro B kata ya Nyankumbu wilayani na mkoani Geita wameiomba serikali kuwasaidia kutafuta suluhu ya kudumu juu ya uhaba wa miundombinu ya barabara hali inayopelekea changamoto ya maji kujaa katika makazi yao pindi mvua zinaponyesha.

Wakizungumza na Storm FM, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameeleza kuwa mvua zinaponyesha hali hiyo imekuwa ikihatarisha usalama wao pamoja na uharibifu wa mali na makazi yao.

Sauti ya wananchi
Diwani wa kata ya Nyankumbu Paschal Sukambi akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula

Diwani wa kata ya Nyankumbu Paschal Kimisha Sukambi amewaomba wataalam mbalimbali kutoka manispaa ya Geita kufika eneo hilo ili waweze kutafuta suluhu ya tatizo hilo.

Sauti ya Paschal Sukambi, Diwani kata ya Nyankumbu
Muonekano wa baadhi ya nyumba za makazi ya watu pindi mvua zinaponyesha. Picha na Ester Mabula

Licha ya malalamiko ya wananchi, kwa mujibu wa maelezo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Geita imeonekana eneo lile ni mkondo wa maji na hivyo ametoa rai kwa wananchi kuzingatia umbali wa mita 60 pindi wanapojenga nyumba za makazi,

Sauti ya Mkurugenzi manispaa ya Geita, Yefred Myenzi
Mkurugenzi manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula