Storm FM
Storm FM
24 February 2026, 9:33 pm

Hadi sasa Jumla ya watu 700 wamefikiwa na huduma ya kupewa miche bure na TFS katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Na: Ester Mabula
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency – TFS) umeendelea kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.
Akizungumza wakati wa ziara katika shule ya msingi Itanga iliyopo wilayani humo, Mhifadhi kutoka TFS Kanda ya Ziwa, Pius Mbila, amewahimiza wananchi na taasisi mbalimbali kuongeza juhudi za upandaji miti ili kuongeza ustawi na maendeleo kwa ujumla
Hata hivyo, Mbila ametaja changamoto zinazokwamisha juhudi hizo kuwa ni pamoja na ukataji holela wa miti, uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kuhusu umuhimu wa miti, pamoja na mtindo wa maisha ukihusishshughuli za kilimo na ufugaji.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kimiti Frank, ameeleza faida za miti shuleni hapo kuwa ni pamoja na kutoa kivuli kwa wanafunzi, kuboresha hewa, kupunguza mmomonyoko wa udongo na kuongeza uzuri wa mazingira ya shule Huku mwalimu wa mazingiraJuma Mathias akieleza jumla ya miti 8000 imepandwa shuleni hapo.

Juma Mathias Shija, amesema awamu ya kwanza ya upandaji miti walianza na miti 2000 mwaka 2019 ambapo wamekuwa na mwendelezo wa kupokea miti kutoka TFS na kwamba zaidi ya miti 8000 imepandwa shuleni hapo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhifadhi Mwandamizi na Kaimu Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Chato, Gerlad Katunzi, ameeleza mikakati ya TFS katika kuendeleza upandaji miti kuwa ni pamoja na ugawaji wa miche bure kwa wananchi, taasisi za serikali na binafsi, pamoja na utoaji wa elimu ya uhifadhi wa misitu, akibainisha kuwa jumla ya watu 700 tayari wamefikiwa kupitia kampeni mbalimbali zinazoendeshwa na TFS wilayani humo.
