Storm FM

Mbunge Lutandula atimiza ahadi ya kununua mitambo ya barabara

17 February 2026, 6:07 pm

“Siwezi kuona wananchi wangu wa Chato kusini wanateseka na miundombinu mibovu ya barabara, na ndiyo maana nilisema ndani ya siku zangu 100 nitaleta mitambo na nimetimiza” – Mbunge Lutandula

Na: Ester Mabula

Mbunge wa Jimbo la Chato kusini Mhe. Paschal Lutandula ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kununua mitambo ya kutengeneza miundombinu ya barabara ndani ya siku 100 za uongozi wake.

Akipokea mitambo hiyo yenye thamani ya shilingi Billioni 1.06 mapema jana Februari 16, 2026 katika hafla iliyofanyika katika kata ya Bwanga amesema alipokuwa akifanya kampeni kilio kikubwa cha wananchi ilikuwa ni miundombinu ya barabara na hivyo uwepo wa mitambo hiyo utasaidia kutatuaa changamoto

Awali akizungumza mgeni rasmi, Katibu wa CCM wilaya ya Chato Dotto Mazuri amesema ni dhamira ya Chama cha Mapinduzi kutatua changamoto na kuboresha miundombinu huku akimpongeza Mbunge kwa hatua hiyo.

Sauti ya mwandishi wetu ikieleza zaidi
Muonekano wa mitambo ambayo imenunuliwa na Mbunge wa kwaajili ya kukarabati barabara. Picha na Ester Mabula

Baadhi ya wananchi wakazi wa jimbo hilo pamoja na Diwani wa kata ya Bwera Josephat Manyenye wamempongeza Mbunge kwa hatua hiyo wakieleza kuwa ameonesha dhamira ya dhati ya kutatua changamoto za wananchi

Muonekano wa mitambo ambayo imenunuliwa na Mbunge wa kwaajili ya kukarabati barabara. Picha na Ester Mabula
Mbunge Lutandula akikabidhi mabati kwaajili ya kuezeka zahanati ya Bukiliguru katika jimbo hilo. Picha na Ester Mabula

Sambamba na hilo Mhe. Lutandula amekabidhi mabati kwaajili ya kukarabati zahanati ya Bukiliguru iliyopo katika Jimbo hilo ambayo ilijengwa kwa muda mrefu bila kuezekwa.