Storm FM

Mradi wa Mama mjamzito na mtoto salama wabisha hodi Geita

13 February 2026, 12:02 pm

Mkurugenzi wa shirika la THAMINI UHAI Bw. Banzi Msumi akizungumza katika hafla ya kuutambulisha mradi mkoani Geita. Picha na Ester Mabula

Shirika la THAMINI UHAI limepata ufadhili wa kutekeleza mradi wa Mama mjamzito na mtoto salama kwa muda wa miaka mitano kuanzia Septemba hadi Juni 2030 kupitia ufadhili wa pamoja wa Bloomberg Philanthropies na Gates Foundation.

Na: Ester Mabula

Shirika la THAMINI UHAI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na ofisi ya waziri mkuu, TAMISEMI linatarajia kutekeleza mradi wa Mama mjamzito na mtoto salama.

Mradi huo utatekelezwa katika mikoa ya Geita, Katavi na Kigoma ambapo unatarajiwa kusaidia katika  kuimarisha huduma za kliniki ya wajawazito, huduma jumuishi za dharura za mama na mtoto ikijumuisha tiba kinga ya kutokwa damu baada ya kujifungua  pamoja na matibabu ya watoto wachanga.

Kwa mkoa wa Geita utatekelezwa katika vituo vya afya viwili, Katoro na Bwanga, akizungumza jana Februari 12, 2026 katika uzinduzi wa mradi huo mkoani Geita, Mkurugenzi wa shirika la THAMINI UHAI Bw. Banzi Msumi hilo ameeleza mambo makuu yatakayotekelezwa katika mradi huo.

Sauti ya mkurugenzi wa shirika Bw. Banza Msumi
Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela akizungumza katika hafla ya kuutambulisha mradi mkoani Geita. Picha na Ester Mabula

Mgeni rasmi, mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amepongeza hatua ya kuwepo kwa mradi huo katika mkoa wa Geita akieleza kuwa utaleta tija pamoja na kuboresha huduma za afya huku mwakilishi kutoka ofisi ya waziri mkuu tamisemi , Idara ya afya, ustawi wa Jamii na Lishe Jesca Tryphone akisisitiza suala la uwajibikaji kwa watumishi wa idara ya afya ili kufikia malengo

Sauti ya RC Geita na mwakilishi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI

Akizungumza baada ya zoezi la uzinduzi na kuutambulisha mradi huo mkoani Geita, Meneja miradi wa shirika la Thamini Uhai, Dkt. Sunday Dominiko amesema mradi huo una thamani ya dola za marekani milioni 12.15 ambapo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano.

Sauti ya meneja miradi wa shirika Dkt. Sunday Dominiko
Baadhi ya watumishi kutoka idara mbalimbali walioshiriki katika hafla ya kuutambulisha mradi mkoani Geita. Picha na Ester Mabula