Storm FM
Storm FM
27 January 2026, 5:10 pm

Baraza la madiwani la halmashauri ya Manispaa ya Geita leo Januari 27, 2026 limejadili na kupitisha rasimu ya bajeti kisasi cha shilingi bilioni 78,811,212,825.7 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Na: Ester Mabula
Bajeti hiyo ina ongezeko la 8.3% zaidi ya ile ya mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo matarajio katika bajeti ya mwaka huu ni kugharamia na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia vipaumbele vilivyotajwa ikiwemo afya, miundombinu ya barabara pamoja na elimu.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya insmanispaa ya Geita Yefred Myenzi ametaja mchanganuo wa bajeti hiyo kwa kuainisha kiwango cha matumizi kwa kila eneo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Geita Leonard Bugomola amewataka madiwani na watendaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii huku akisema ukuaji wa manispaa uendane sambamba na uvumbuzi wa vyanzo vipya vya mapato kupitia miradi mbalimbali.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita Bi. Lucy Beda ameipongeza halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa juhudi zake za kuendelea kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo akisema hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma kwa wananchi na kuleta tija katika matumizi ya rasilimali za UMMA.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Reuben Sagayika ambaye ni diwani wa kata ya Kalangalala amepongeza bajeti hiyo akieleza kuwa imelenga maeneo muhimu kwa wananchi.
