Storm FM

Katukula afariki akiwa na miaka 115, aacha familia ya watu 1,989

26 January 2026, 1:15 pm

Muonekano wa picha ya mzee Jacob Chigabilo (enzi za uhai wake) katika ibada ya kuaga mwili wake. Picha na Kale Chongela

“Tunashukuru malezi na mafundisho aliyotupa baba yetu na tutayaendeleza kwa uzao wake ikiwa ni kuendelea kuheshimu watu wote katika Jamii” – Mtoto wa marehemu

Na: Kale Chongela

Historia ya kuishi duniani ya Mzee Jacob Chigabilo Katukula mkazi wa mtaa wa Nyamakale kata ya Nyankumbu, halmshauri ya manispaa ya Geita mwenye umri wa miaka115 imefikia tamati Januari 19, 2026 baada ya kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Wakazi wa Geita wameungana na familia katika ibada maalum ya kumuaga mpendwa wao Mzee Chigabilo ibada ambayo imefanyika  nyumbani kwa marehemu ambapo ibada hiyo imeongozwa na Padri  Silas Haki kutoka parokia ya Mtakatifu Antony wa Padua Nyarubele.

Mzee Chigabilo ameacha watoto 34, wajukuu 206, vitukuu 624, vilembwe 1009, vilembwekeze 116.

Taarifa ya Kale Chongela inaeleza zaidi.

Sauti ya ripoti zaidi
Jeneza lenye mwili wa marehemu katika ibada ya kumuaga iliyofanyika nyumbani kwa marehemu. Picha na Kale Chongela
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo watoto, wajukuu, vitukuu, vilembwe na vilembwekeze. Picha na Kale Chongela