Storm FM
Storm FM
20 January 2026, 12:50 pm

Jumla ya miradi 901 yenye thamani ya Tsh. bilioni 9.31 kwa mwaka 2024, na miradi 927 kwa mwaka 2025 yenye thamani ya Tsh. bilioni 11 ambapo jumla ya miradi 469 inamilikiwa na watanzania sawa na asilimia 51%.
Na: Ester Mabula
Watanzania wametakiwa kuendelea kutumia fursa za uwekezaji zilizizopo nchini sambamba na kusajili miradi yao kwenye mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalumu ya kiuchumi (TISEZA) hatua itakayowawezesha kukua, kupata tija ya kiuchumi na kupata nafuu ya msamaha wa kodi kwa bidhaa ambazo zinatumika kwenye miradi iliyosajiliwa.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa TISEZA, Dkt. Aziz Ponary Mlima jana Januari 19, 2026 akiwa katika ziara mkoani Geita ya kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji uwekezaji wa ndani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa miaka mitano (FYDP) inayolenga kutekeleza azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kufungua nchi kwa kuhamasisha uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela akizungumza mapema na uongozi wa TISEZA amepongeza uwepo wa ziara hiyo inayolenga kupita mikoa mbalimbali nchini ili kujenga uelewa akieleza hatua hiyo itasaidia kuamsha ari ya wananchi kujisajili.

Mwekezaji katika sekta ya uchimbaji wa dhahabu mkoani Geita ambaye pia ni mmiliki wa hoteli, Leonard Bugomola amewasihi watanzania kusajili miradi yao akieleza manufaa anayopata huku mwekezaji wa uchenjuaji wa dhahabu Bi. Zahida Abdalah akiipongeza serikali kwa kuendelea kurahisisha michakato ya upataji vifaa mbalimbali kwaajili ya shughuli zao

Pamoja na ziara hiyo ya kukagua miradi ya wawekezaji, mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalumu ya kiuchumi (TISEZA) pia itaendesha semina na makongamano ya Uwekezaji kwa makundi mbalimbali katika jamii yanayojumuisha wajasiriamali wadogo na wa Kati (SMEs), wafanyabiashara, vijana, wanahabari, maafisa wanaosimamia viwanda, biashara na uwekezaji katika sekretarieti za mikoa na halmashauri.
