Storm FM
Storm FM
16 January 2026, 5:28 pm

Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole amekuwa na utaratibu wa kutoa madaftari kwa wanafunzi wakidato cha kwanza katika shule 2 za sekondari zilizopo katika kata hiyo.
Na: Ester Mabula
Wananchi wa mtaa wa Nyakato kata ya Nyanguku, halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita wamemshukuru Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole kwa kuweza kutoa madaftari kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Nyakato.
Wananchi hao wameeleza kumuunga mkono diwani huyo kwa kuhakikisha watoto wanakwenda shule sambamba na kushiriki kikamilifu michango ya shule ikiwemo kulipa walimu wa kujitolea.
Jumla ya wanafunzi 69 wa kidato cha kwanza wanatarajiwa kuripoti katika shule hiyo, ambapo hadi leo ni wanafunzi 44 wameripoti na kupewa madaftari aina ya counter book 10 kila mmoja ikiwa ni utaratibu wa diwani huyo kutoa madaftari kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kila mwaka katika shule za sekondari 2 zilizopo katika kata hiyo ambazo ni Nyanguku na Nyakato.

