Storm FM
Storm FM
14 January 2026, 10:41 am

“Jamani mtu kama unaona kakosea ni bora kumpeleka kwenye mamlaka husika na sio kumpiga na kumtelekeza kama hivi” – Mwananchi
Na: Ester Mabula
Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 ambaye ameshindwa kuzungumza vizuri huku akishindwa kutaja jina lake amedai kupigwa na watu usiku akihisiwa kuwa ni mwizi.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Januari 13, 2026 ambapo kijana huyo amekutwa akiwa amelala katika uwanja wa mpira wa shule ya sekondari Nyanza, mtaa wa Nyanza, halmashauri ya manispaa ya Geita ambapo ameshindwa kuzungumza akidai kuishiwa nguvu.

Wakizungumza baadhi ya wananchi ambao walijitokeza kushuhudia tukio hilo Lucas John na Elizabeth Mihayo wameeleza namna walivyomuona mtu huyo

Hamis abdallah ni Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyanza ameeleza hatua walizochukua juu ya tukio hilo ambapo amesema walihusisha Jeshi la polisi kwa hatua zaidi.
Viongozi wa serikali ya mtaa akiwemo Mwenyekiti walifanya jitihada za kulifikia Jeshi la poisi kwa hatua zaidi ambapo hata hivyo Jeshi la polisi limefika eneo la tukio na kumchukua kijana huyo kwa msaada zaidi.
