Storm FM
Storm FM
12 January 2026, 4:38 pm

Zaidi ya wanafunzi 600 wamepewa madaftari na Diwani wa kata ya Kalangalala ikiwa ni mpango wa kuhakikisha wanafunzi wanakwenda shuleni bila kuwa na kikwazo cha ukosefu wa madaftari.
Na: Ester Mabula
Wananchi wa kata ya Kalangalala halmashauri ya manispaa ya Geita, mkoani Geita wametoa pongezi na shukrani kwa Diwani wa kata hiyo Reuben Sagayika kwa kuweza kuwasaidia madaftari pamoja na kalamu kwaajili ya kuanza muhula mpya wa masomo hapo kesho Januari 13, 2026.
Wakizungumza na Storm FM leo Januari 12, 2026, Bi. Consolata Lwanga na Yohanna Benjamin ambao ni wakazi wa kata hiyo wamesema hatua hiyo inalenga kuleta hamasa kwa wazazi kupeleka watoto shule huku wakiwaomba viongozi wengine kuiga mfano huo.
Afisa Elimu kata ya Kalangalala Bi. Regina Cosmas Ketau amesema mpango huo ulilenga kutoa madafatri kwa watoto 600 huku Afisa mtendaji wa kata ya Kalangalala Bw. Emmanuel Bomani akieleza kuwa hatua hiyo ni endelevu ambayo inalenga kutoa motisha kwa wanafunzi kuendelea na masomo

Akizungumza na wazazi waliojitokeza katika zoezi hilo la ugawaji madaftari, Diwani Reuben Sagayika amesema mpango huo ni endelevu kwani dhamira yake ni kuendelea kutatua changamoto za wananchi wake.
