Storm FM
Storm FM
10 January 2026, 6:38 pm

Januari 13, 2026 shule zote nchini zitafunguliwa na kuanza rasmi kwa mhula mpya wa masomo baada ya kukamilika sikukuu za mwisho wa mwaka.
Na: Ester Mabula
Diwani wa kata ya Kalangalala wilayani na mkoani Geita Reuben Sagayika leo Januari 10, 2026 amefanya ziara ya kutembelea shule ya msingi Kalangalala ili kufuatilia zoezi la uandikishaji wanafunzi shuleni hapo kwa ajili ya mhula mpya wa masomo unaotarajiwa kuanza Januari 13, 2026.
Akiwa shuleni hapo Sagayika ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto atakuwa na zoezi la kugawa vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji siku ya Jumatatu Januari 12, 2025 ambapo zoezi hilo litafanyika katika ofisi ya kata hiyo.

Aidha ameeleza kuwa ziara za kutembelea shule zilizopo katika kata hiyo ni zoezi endelevu ambalo litasaidia kuweza kubaini changamoto zilizopo kwenye shule hizo kwaajili ya utatuzi.

Kaimu Afisa Elimu kata ya Kalangalala Regina Comas Ketau ameeleza kuwa kata hiyo ina jumla ya shule 9 za msingi ambapo hadi sasa jumla ya wanafunzi 1640 wameandikishwa huku kukiwa na matarajio makubwa ya kuandikisha kwa asilimia 100.

Kaimu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kalangalala Mwl. Sospter Luzige amewasisistiza wazazi kupeleka watoto kuandikisha na kuacha kuwapeleka katika shule za mitaani huku Katibu wa Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya kalangalala Richard Nzagamba wa akitoa pongezi kwa Diwani huyo kwa kuw]akumbuka wanafunzi wenye uhitaji.
