Storm FM
Storm FM
8 January 2026, 7:01 pm

“Lengo ni kuhakikisha abiria na watumiaji wa barabara wanakuwa katika hali ya usalama pindi wanapotumia stendi hii hususani kipindi cha mvua” – Reuben Sagayika
Na: Ester Mabula
Wananchi na watumiaji wa kituo kikuu cha mabasi mkoa wa Geita wameishukuru serikali kwa kushirikiana na Diwani wa kata ya Kalangalala kwa kuchukua hatua ya kufukia mashimo yaliyokuwa yakisababisha usumbufu mkubwa kwa muda mrefu.
Mashimo hayo yalitokana na uharibifu wa miundombinu kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha, hali inayosababisha usumbufu wakati wa utumiaji wa kituo hicho cha mabasi.

Wakizungumza na Storm FM wameipongeza serikali na kumshikuru diwani kwa kuchukua hatua kwa haraka ya kutatua kero hiyo kama anavyobainisha mwenyekiti wa stedni hiyo Godfrey Joseph.
Mmoja wa madereva pamoja na abiria ameeleza hatua hiyo iliyochukuliwa itasaidia kupunguza usumbufu kwa madereva pamoja na abiria.

Diwani wa Kata ya Kalangalala, Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Mhe. Reuben Sagayika mapema leo Januari 08, 2025 ametembelea stendi hiyo na kujionea hatua za marekebisho zinazoendelea akisema lengo ni kuhakikisha stendi inakuwa salama na rafiki kwa watumiaji wote, hasa katika kipindi cha mvua.