Storm FM
Storm FM
27 December 2025, 4:57 am

“Kila mwaka zoezi la uandikishaji huanza mwezi Septemba na kukamilika tarehe 31, marchi ili kutoa nafasi kwa wazazi na walezi kuandikisha watoto wao” – Afisa elimu mkoa wa Geita
Na: Ester Mabula
Afisa elimu mkoa wa Geita Mwalimu Antony Mtweve ametoa rai kwa wazazi na walezi mkoani Geita kuendelea na zoezi la kuandikisha wanafunzi kwa ajili ya muhula mpya wa masomo 2026.
Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Storm FM akiwa ofisini kwake na kueleza kuwa zoezi la uandikishaji limeanza tangu mwezi Septemba na litakamilika mwezi marchi, 2026.

Akizungumzia hali ya uandikisaji kwa ngazi ya halmashauri, amesema halmashauri ya wilaya Nyangh’wale inaongoza kwa kuandikisha wanafunzi 5368 sawa na asilimia 73 kwa wanafunzi wapya wa elimu ya awali na wanafunzi 6539 sawa na asilimia 87 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza
Aidha Afisa elimu mkoa wa Geita ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kujitokeza kuandikisha wanafunzi mapema ili kuondoa changamoto za kuchelewa kuanza masomo.