Storm FM
Storm FM
26 December 2025, 2:07 am

“Ofisi ya mbunge jimbo la Chato Kusini itaendelea kushirikiana na wananchi katika mambo mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya jimbo letu” – Joseph James, Katibu wa Mbunge
Na: Ester Mabula
Mbunge wa Jimbo la Chato kusini Paschal Lutandula amewakumbuka wagonjwa wanaopatiwa huduma katika kituo cha Afya Bwanga kwa kuwaandalia chakula cha pamoja na kuwakabidhi mahitaji mbalimbali.
Mahitaji hayo yamekabidhiwa Disemba 25, katika maadhimisho ya sikukuu ya Christmass, katika kituo cha Afya Bwanga ambapo makabidhiano yameongozwa na Diwani wa Kata ya Bwanga Bw. Sanane Chai ambaye ametoa wito kwa viongozi wengine kuendelea kuikumbuka Jamii kwa mahitaji mbalimbali.

Akizungumza Dkt. Enos Kasongi, ambaye ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bwanga ameeleza jumla ya watoto 16 wamezaliwa sikukuu ya christmass katika kituo hicho na kutoa pongezi kwa mbunge kwa kuweza kuikumbuka Jamii.
Baadhi ya wagonjwa ambao ni akina mama waliojifungua watoto akiwemo Fatuma Hamis na Ester Bukeye wamepongeza hatua hiyo na kumshukuru kwa kuweza kuwakumbuka katika siku hiyo muhimu ya Christmas.

Katibu wa Mbunge Joseph James amesema hatua hiyo imelenga kurejesha tabasamu kwa wananchi wa Chato kusini na kwamba ofisi ya Mbunge itaendelea kushirikiana na wananchi katika Nyanja mbalimbali.
