Storm FM

Mkandarasi akaliwa kooni Geita

17 December 2025, 9:30 pm

Mkuu wa mkoa wa Geita siku chache baada ya kikao cha bodi ya barabara alipotembelea mradi barabara za kilometa 17 Geita mjini. Picha na Mrisho Sadick

Katika mwaka wa fedha 2025/2026 walitengewa jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya aina mbalimbali ya barabara na madaraja

Na Mrisho Sadick:

Serikali mkoani Geita imetangaza rasmi kuanza kumkata fedha mkandarasi anayejenga barabara za lami zenye urefu wa kilometa 17 Geita mjini zinazogharimu zaidi ya bilioni 22za mradi wa TACTIC huku akiiagiza Manispaa ya Geita kuanza mchakato wa kutafuta mkandarasi mwingine atakaemalizia mradi huo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Geita cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara na madaraja pamoja na miradi ya maendeleo kuanzia mwezi machi  hadi disemba 2025.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara. Picha na Mrisho Sadick

Kwenye kikao hicho meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Mhandisi Vedastus Maribe amesema Katika mwaka wa fedha 2025/2026 walitengewa jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya aina mbalimbali ya barabara na madaraja huku akieleza changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo ni pamoja na wizi na uharibifu wa miundombinu huku akiomba ushirikiano wa karibu kukabiliana na hali hiyo.

Sauti ya meneja wa TANROADS
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Nyarugusu wilayani Geita wameendelea kuikumbusha serikali kuharakisha mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Geita Nyarugusu hadi kahama kwakuwa wanaitegemea sana kiuchumi kwakuwa eneo hilo lina shughuli nyingi za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Sauti ya Wananchi Nyarugusu
meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Mhandisi Maribe akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha bodi ya barabara, Picha na Mrisho Sadick