Storm FM

Moto wa ajabu wateketeza samani za ndani Geita

5 December 2025, 2:03 pm

Muonekano wa mali zilizoteketea kwa moto ndani ya chumba Nyantorotoro A . Picha Kale Chongela

Hakuna madhara ya kibinadamu kwakuwa jitihada kubwa zilifanyika kuuzima moto huo kwa kushirikiana na majirani.

Kale Chongela:

Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza vitu vya ndani katika chumba cha Bw. David Pankras, mkazi wa Mtaa wa Nyantorotoro A Kata ya Nyankumhu, Manispaa ya Geita.

Bw. David akizungumza na Storm FM amesema kuwa wakati moto unatokea hakuwepo nyumbani, na mke wake alikuwa ameenda kwenye vikundi vyao. Ameeleza kuwa licha ya jitihada kubwa kufanyika za kuzima moto, hazikuzaa matunda kwani moto ulikuwa mkubwa.

Sauti ya Mmiliki wa Chumba
Muonekano wa mali zilizoteketea kwa moto ndani ya chumba Nyantorotoro A . Picha Kale Chongela

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema jitihada kubwa zilifanyika za kuzima moto kwa kushirikiana na majirani, ndipo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likafika na kuanza kusaidia katika kuzima moto huo.

Sauti ya Mashuhuda

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Mrakibu Msaidizi Hamis Shabani Dawa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa limetokea mnamo tarehe 02 Desemba 2025, na kwamba mmiliki wa nyumba hiyo ametambuliwa kwa jina la Sarah Benjamini.

Sauti ya Kamanda wa Zimamoto