Storm FM
Storm FM
4 December 2025, 5:19 am

Kila Jumatano ya kwanza ya mwezi, mamlaka ya huduma za nishati na maji nchini (EWURA) hutangaza bei kikomo za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.
Na: Ester Mabula
Taarifa iliyotolewa Jumatano ya Disemba 03, 2025 nz Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) imeainisha bei elekezi kwa kila mkoa nchini ambazo zitatumika kwa mwezi huu wa Disemba.
Kwa mkoa wa Geita bei za Petroli na Dizeli ni kama ifuatavyo;
-Kwa wilaya ya Geita Petrol ni 2,950 na Dizeli ni 2,980 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Bukombe Petrol ni 2,939 na Dizeli ni 2,969 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Chato Petrol ni 2,971 na Dizeli ni 3,001 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Mbogwe Petrol ni 2,988 na Dizeli ni 3,018 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Nyang’hwale Petrol ni 2,965 na Dizeli ni 2,995 kwa lita moja.
Utofauti wa bei hizo na bei za mwezi Novemba ni kama ifuatavyo
-Kwa wilaya ya Geita Petrol ni 2,952 na Dizeli 2,905 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Bukombe Petrol ni 2,941 na Dizeli 2,894 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Chato Petroli ni 2,973 na Dizeli 2,926 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Mbogwe Petrol ni 2,990 na Dizeli 2,943 kwa lita moja.
-Kwa wilaya ya Nyang’hwale Petrol ni 2,967 na Dizeli 2,920 kwa lita moja.