Storm FM
Storm FM
2 December 2025, 7:32 pm

Baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Geita limeketi leo Disemba 02, 2025 katika kikao cha kwanza ambapo lilianza kwa zoezi la madiwani wateule kula viapo vya utumishi.
Na: Ester Mabula
Diwani wa kata ya Kalangalala Reuben Sagayika mara baada ya kula kiapo ameahidi kutimiza yale yote aliyonadi wakati wa kampeni sambamba kueleza kuwa atakuwa “Sauti ya Kalangalala” akisisitiza katika uongozi wa uwazi na ushirikishwaji wananchi wa rika zote.
Katika kikao hicho cha baraza la madiwani kiliongozwa na ajenda mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa baraza, viapo vya maadili, uchaguzi wa mstahiki meya na naibu meya pamoja na uundwaji wa kamati za kudumu katika idara mbalimbali.
