Storm FM
Storm FM
30 November 2025, 2:35 pm

Iwapo wananchi hawatachukua hatua za haraka za kujitokeza kufanya uchunguzi wa magonjwa yasioambukiza yanaweza kuleta madhara makubwa ikiwemo figo kufeli.
Na Mrisho Sadick:
Chama cha ugonjwa wa kisukari Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Geita kimetoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Geita na Chato kuendelea kubadili mtindo wa maisha usiofaa kuanzia ngazi ya kaya ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo mara nyingi hujitokeza bila dalili.
Wito huo umetolewa na Mashombo Mkambakutoka chama hicho makao makuu Jijini Dar es salaamkatika Kata ya Bwangasiku ya pili ya zoezi la uchunguzilililowahusisha zaidi ya watu 600 waliojitokeza kupatiwa huduma amesema iwapo wananchi hawatachukua hatua za haraka za kujitokeza kufanya uchunguzi, magonjwa hayo yanaweza kuleta madhara makubwa ikiwemo figo kufeli, matatizo ya mishipa ya damu, kupoteza uoni na madhara mengine makubwa yanayoweza kuepukika endapo uchunguzi utafanyika mapema.
Watoa huduma ngazi ya jamii pamoja na wakazi wa Kata ya Bwanga walioshiriki katika zoezi hilo wamekiri kuwepo kwa changamoto ya ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza, na wakahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kupima mara kwa mara, hasa baada ya serikali kuanzisha kliniki ya kudumu katika Kituo cha Afya Bwanga.

Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza wilayani Chato, Dkt. Alexander Mpondaguzi, amesema uanzishwaji wa kliniki hiyo umechochewa na kampeni zinazofanywa kila mwaka na Chama Cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania huku akizitaja takwimu za mwaka jana katika zoezi la aina hiyo kuwa kati ya watu zaidi ya 500 waliopimwa, asilimia 7.6 walibainika kuwa na kisukari na asilimia 39.7 walikuwa na shinikizo la juu la damu.