Storm FM

Watoto wenye udumavu Bukombe wapungua

24 November 2025, 3:41 pm

Mkuu wa wilaya ya Bukombe akitoa zawadi kwa mwanafunzi katika maadhimisho ya lishe Bukombe. Picha na Mrisho Sadick

Walimu na maafisa kilimo kushirikiana kuongeza uzalishaji wa chakula shuleni kupitia mashamba ya shule

Na Mrisho Sadick:

Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 86 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026 hali ambayo imeendelea kusaidia kupunguza idadi ya watoto wenye udumavu wilayani humo kutoka watoto 23 hadi 15 kwa mwaka.

Baadhi ya wananchi wilayani Bukombe wakiwa kwenye maadhimisho ya lishe. Picha na Mrisho Sadick

Akitoa takwimu za kupungua kwa udumavu huo kwa mwaka 2023/2024 na 2025/2025 kwenye maadhimisho ya siku ya lishe wilayani Bukombe, afisa lishe wa wilaya hiyo amesema serikali imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wananchi pamoja na kutenge fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli za lishe.

Baadhi ya vyakula vikiwa katika maadhimisho ya lishe kwa ajili ya elimu kwa wananchi Bukombe. Picha na Mrisho Sadick

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukombe Bi Adelina Mfikwa amewahimiza walimu na maafisa kilimo kushirikiana kuongeza uzalishaji wa chakula shuleni kupitia mashamba ya shule ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na udumavu.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Paskasi Muragili akiwa kwenye maadhimisho hayo ameitaka jamii kuzingatia masuala ya lishee kuanzia mtoto akiwa tumboni hadi makuzi yake.

Sauti ya ripoti kamili ya stori hii