Storm FM
Storm FM
18 November 2025, 12:21 pm

Fursa ya ufugaji wa Samaki kwa kutumia vizimba iliyokuwa haitazamwi sana kwasasa imekuwa kimbilio
Na Mrisho Sadick:
Serikali Mkoani Geita imewataka maafisa maendeleo kuhakikisha wanakuwa daraja muhimu la kuwakwamua Wananchi kiuchumi kwa kuibua fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye maeneo yao ikiwemo ufugaji wa Samaki kupitia vizimba.
Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Mohamed Gombati ametoa maagizo hayo kwenye Kongamano la kwanza la maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Geita lililofanyika Manispaa ya Geita huku afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Geita Martha Kaloso akisema kongamano hilo litakwenda kuongeza uwajibikaji kwa jamii kwa maafisa maendeleo hao.

Kwa upande wake Carlos Gwamagobe Kutoka Wizara ya maendeleo ya Jamii amewataka maafisa maendeleo hao kuendelea kuwasaidia wananchi kuchangamkia fursa zingine za uchumi siyo kutegemea shughuli za uchimbaji wa madini pekee.

Maafisa maendeleo wanaotoka Kata zinazopakana na ziwa Victoria wamesema fursa ya ufugaji wa Samaki kwa kutumia vizimba iliyokuwa haitazamwi sana kwasasa imekuwa kimbilio Kutokana na Elimu ambayo wanaendelea kuitoa.
Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni – Uchechemuzi ni dira ya matokeo chanya kwa Jamii.