Storm FM
Storm FM
13 November 2025, 1:50 pm

Suala la wananchi wa Butengorumasa kujitolea kwa hiari yao kuanzisha ujenzi wa Zahanati imekuwa mkombozi kwao baada ya TFS kuingilia kati nakukamilisha ujenzi huo.
Na Mrisho Sadick:
Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji cha Butengorumasa wilayani Chato Mkoani Geita wamekamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho nakuwaondolea changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya vijiji jirani.
Kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hiyo nakuanza kutoa huduma iliwasukuma wakazi wa Kijiji hicho kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti Silayo kuanzisha ujenzi wa Nyumba ya watumishi ambayo hadi kukamilika kwakwe itagharimu zaidi ya milioni 70.

Mhifadhi mkuu wa shamba la miti silayo Juma Mseti amesema katika kuunga mkono jitihada za wananchi wamechangia milioni 85 za ukamilishaji wa Zahanati pamoja na milioni 79 kwa ajili ya ukamilishaji wa Nyumba ya Watumishi katika Zahanati hiyo.

Akiwa kwenye ukaguzi wa miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewapongeza wananchi pamoja TFS kwa hatua hiyo huku akiwaahidi kuwa serikali itaendelea kupeleka mahitaji muhimu katika Zahanati hiyo.