Storm FM
Storm FM
20 October 2025, 12:51 pm

Hii ni awamu ya nne kupokea madakari bingwa wa mama samia nakwamba katika awamu zilizopita zaidi ya watu 10,000 walifikiwa na huduma hizo.
Na Mrisho Sadick:
Mkoa wa Geita umepokea madaktari Bingwa 42 kutoka kambi ya Mama Samia watakaotoa huduma ya matibabu ya kibingwa katika halimashauri zote sita za mkoa wa Geita kwa kuanzia leo Oktoba 20 hadi 24 mwaka huu.
Madaktari hao wamepokelewa leo Oktoba 20 na Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita Dkt Omari Sukari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ambapo amesema watakwenda kutoa huduma kwenye vituo saba katika halmashauri zote sita za mkoa wa Geita.
Dkt Sukari amesema kwa mkoa wa Geita hii ni awamu ya nne kupokea madakari bingwa wa mama samia nakwamba katika awamu zilizopita zaidi ya watu 10,000 walifikiwa na huduma hizo huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika Hospitali za wilaya na vituo vilivyoelekezwa kwa ajili ya kupata huduma za kibingwa.

Kwa upande wake Paskalina Mahu kutoka wizara ya afya ambaye ni Mratibu wa zoezi la Dkt Samia Mentership kwa mkoa wa Geita amewataka madaktari hao kwenda kushirkiana na watalaamu watakao wakuta kwenye vituo hivyo ikiwemo kuwajengea uwezo.

Baadhi ya madaktari wametoa wito kwa wananchi Mkoani Geita kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo kwakuwa haipatikani kila siku kwenye maeneo yao.