Storm FM
Storm FM
18 October 2025, 4:47 am

“Hatutakubali kuona waganga wenye nia ovu wanaendelea kuiangamiza Jamii, na hili linaanza na nyie wenyewe kwa kuhakikisha kila mmoja wenu anasajiliwa” – SACP Safia Jongo
Na: Kale Chongela
Jeshi la Polisi mkoani Geita limesema halitawafumbia macho baadhi ya waganga wa tiba asili wanaotumia ramli chonganishi zinazopelekea kuwa chanzo cha migogoro katika Jamii ya mkoa wa Geita.
Hayo yamebainishwa Oktoba 1, 2025 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Safia Jongo wakati wa kikao na waganga wa tiba asili kilichofanyika katika uwanja wa Dkt. Samia Suluhu mtaa wa Bombambili manispaa ya Geita ambapo amewasihi kuwa mstari wa mbele katika kueneza amani na upendo.
Mara baada ya kikao hicho, baadhi ya waganga wa tiba asili wamesema baadhi yao si wanachama bali wamekuwa wakifanya kazi hiyo kinyume na utaratibu huku wakiahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukomesha suala hilo.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ametumia fursa hiyo kuwataka waganga wa tiba asili kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata kanuni na taratibu akisisitiza zaidi kujisajili.
