Storm FM

UWT kusaka kura milioni 16 za Dkt. Samia

18 September 2025, 7:22 pm

Mwenyekiti wa UWT Taifa Merry Chatanda akizungumza na wajumbe wa jumuiya hiyo Geita. Picha na Mrisho Sadick

Zaidi ya wanawake 700,000 wamejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura Mkoani Geita hali ambayo inawapa matumaini UWT

Na Mrisho Sadick:

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) imeweka mkakati wa kutafuta kura milioni 16 kwa ajili ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Mkakati huo umetangazwa leo Septemba 18,2025 na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Merry Chatanda, wakati akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo, wagombea udiwani, ubunge pamoja na makundi mbalimbali ya wanawake katika kikao kilichofanyika Manispaa ya Geita.

Sauti ya Mwenyekiti UWT Taifa
Katibu wa CCM Mkoa wa Geita Alexandrina Katabi akizungumza kwenye mkutano wa mwenyekiti wa UWT Taifa mjini Geita. Picha na Mrisho Sadick

Katibu wa CCM Mkoa wa Geita Alexandrina Katabi amesema wanataka kura za Dkt Samia ambazo hazina mashaka nakuwataka wanawake wote wa UWT Mkoa wa Geita kuhakikisha wanakwenda kuhamasishana kuhakikisha kila mmoja ajitokeze kupiga kura Oktoba 29,2025

Sauti ya Katibu wa CCM Mkoa wa Geita

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita, Lolensia Bukwimba, amesema zaidi ya wanawake 700,000 wamejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuahidi kuhakikisha wote wanashiriki kupiga kura ili kufanikisha azma hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita
Wajumbe wa UWT Mkoa wa Geita wakiwa kwenye mkutano wa mwenyekiti wa umoja huo taifa. Picha na Mrisho Sadick

Katika hatua nyingine Chatanda amewataka Wabunge na Madiwani wa vitimaalumu walioteuliwa na Chama hicho hususan wale walioko kwenye kipindi cha nne kuhakikisha wanatoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM kila baada ya miezi minne, ili wananchi waone hatua zinazochukuliwa na chama chao katika kuwaletea maendeleo.