Storm FM
Storm FM
16 September 2025, 11:10 am

Vyama mbalimbali vya siasa nchini vimeendelea na kampeni ikiwa ni njia ya kunadi sera na mipango yao kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Na: Edga Rwenduru
Chama cha United Democratic Party (UDP) kimewaahidi watanzania kusimamia rasilimali za nchi kwa uzalendo ili kila mwananchi afaidike na uwepo wa rasilimali hizo.
Akiwa mkoani Geita, mgombea wa kiti cha urais kupitia chama hicho Saumu Rashid ameahidi kuwa iwapo chama chake kitapewa dhamana ya kuongoza nchi, serikali yake itaweka mkazo katika kuinua uchumi wa Watanzania pamoja na kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha zaidi wananchi.

Kwa upande wake, mgombea mwenza wa urais kupitia chama cha UDP, Juma Hamis Faki, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kwani ni zoezi la kidemokrasia.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita aliojitokeza kusikiliza sera za chama cha UDP wameeleza kuridhishwa na sera za mgombea huyo.
