Storm FM
Storm FM
16 September 2025, 7:39 am

Mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda, wilaya ya Geita kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif, amezindua rasmi kampeni zake Septemba 15, 2025 kwa kuahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi.
Na: Ester Mabula
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyarugusu, iliyopo kata ya Nyarugusu, Dkt. Jafari amewaomba wananchi wamchague kwa kura nyingi ili aweze kuwatumikia kwa ufanisi.
“Ilani ya CCM imeeleza mengi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kutoka hapa Nyarugusu kwenda hospitali ya wilaya. Ninawaahidi ndugu zangu, nitasimamia kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kikamilifu,” alisema Dkt. Jafari.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Geita, Elivalist Gervas, aliwahimiza wananchi wa Busanda kumuunga mkono Rais Dkt. Samia, pamoja na kuwapigia kura za kishindo wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya ubunge hadi udiwani katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
