Storm FM
Storm FM
15 September 2025, 12:39 pm

“Tunawashuru walimu kwa kutuandalia safari hii kwani imekuwa yenye tija kwetu katika kufahamu tabia za wanyama” – Mwanafunzi
Na: Kale Chongela
Wanafunzi wa shule ya msingi Mkoani iliyopo kata ya Kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita wametembelea shamba la wanyama pori lililopo wilaya ya Chato mkoani Geita lenye ukubwa wa ekari 2500.
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wanafunzi ambao wametembelea shamba hilo la wanayama pori wamesema fursa hiyo imewajengea uelewa juu ya mambo mbalimbali kuhusu wanyama ikiwemo kufahamu namna ambavyo maisha ya wanyama yalivyo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mkoani Mwl. Hubert Revelian amesema lengo la kuwapelekea wanafunzi katika shamba hilo la wanyama pori ni kuwasaidia kujifunza kwa vitendo juu ya wanyama pori.

Mhifadhi wa wanyama pori katika shamba hilo Bw. Seithi Elias Mashini amesema katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 2500 wapo wanyama mbalimbali ikiwemo twiga, pundamilia, swala na ngiri huku akiwasihi wananchi kutembelea shamba hilo la wanyama pori.
