Storm FM
Storm FM
12 September 2025, 4:49 am

“Kwakweli tunampongeza Rais Samia kwa kutukumbuka kwenye hili kwani tulikuwa tunapitia changamoto sana kupata huduma za Afya” – Mwananchi
Na: Kale Chongela
Wakazi wa mtaa wa Ibolelo maarufu Mwabasabi kata ya Nyankumbu, halmashauri ya manispaa ya Geita wameipongeza serikali kwa kuwajengea zahanati katika mtaa huo.
Wakizungumza na Storm FM Septemba 10, 2025 baadhi ya wananchi wakiwa katika eneo ilipo zahanati hiyo wameeleza kuwa zahanati hiyo itatatua changamoto ya kutembea umbali mrefu kwani hapo awali walikuwa wakienda katika kituo cha afya Nyankumbu.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Juma Ramadhan Ruge amefafanua kuwa zahanati hiyo imejegwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja na kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita imejikita katika kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
