Storm FM
Storm FM
4 September 2025, 10:38 am

Mwenge wa uhuru ukiwa wilaya ya Nyangh’wale umetembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye jumla ya miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.
Na: Kale Chongela
Mwenge wa uhuru umeridhishwa na ujenzi wa mradi wa visima vitano vya maji katika kata ya Shabaka, halmashauri ya wilaya ya Nyangh’wale vinavyotarajiwa kuondoa changamoto ya maji kwa wakazi wa eneo hilo.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Ismail Ally Ussi baada ya kukagua mradi huo ameridhishwa na utekelezaji wa mradi na kwamba ipo haja ya wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi katika kulinda miundombinu ya maji ili iweze kuduma kwa muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Grace kingalame ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika wilaya hiyo ili kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa RUWASA Mhandisi Suzana Gogadi amesema vijiji vitano vitanufaika na mradi huo wa maji na kwamba umegharimu zaidi ya shilingi milioni 300.
Taarifa ya mwandishi wetu Kale Chongela inafafanua zaidi.