Storm FM
Storm FM
3 September 2025, 9:53 am

Kila Jumatano ya kwanza ya kila mwezi mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) hutangaza bei kikomo za mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa.
Na: Ester Mabula
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini EWURA imetangaza bei mpa kikomo za mafuta kwa mwezi Septemba, 2025.
Katika wilaya za Mkoa wa Geita bei mpya za mafuta ni kama ifuatavyo:
Wilaya ya Geita Petroli ni 3,007 kwa lita na Dizeli ni 2955
Wilaya ya Bukombe Petroli ni 2996 kwa lita na Dizeli ni 2944
Wilaya ya Chato Petroli ni 3028 kwa lita na Dizeli ni 2976
Wilaya ya Mbogwe Petroli ni 3,045 kwa lita na Dizeli ni 2993
Wilaya ya Nyang’hwale Petroli ni 3,022 kwa lita na Dizeli ni 2970