Storm FM
Storm FM
23 August 2025, 9:28 pm

Kikao cha Halmashuri Kuu ya CCM Taifa cha uteuzi wa wagombea kimeongozwa na mwenyekiti wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan.
Na Mrisho Sadick:
Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Amos Makalla ametangaza majina ya wagombea Ubunge katika majimbo tisa ya Mkoa wa Geita baada ya kikao cha uchujaji cha Kamati Kuu ya CCM kumaliza kazi yake.
Makalla ametangaza majina hayo leo agosti 23,2025 makao makuu ya chama hicho Jijini Dodoma ambapo amewataja walioteuliwa kuwa ni Dkt Doto Biteko Jimbo la Bukombe , Chacha Wambura Jimbo la Geita mjini, Joseph Musukuma Jimbo la Geita,Kija Ntemi Jimbo la Katoro , Dkt Jafari Seif Jimbo la Busanda.

Wengine ni Paschal Lutandula Jimbo la Chato Kusini , Cornel Magembe Jimbo la chato kaskazini ,Nassoro Amar Kasu Jimbo la Nyangh’wale na Fagason Massasi Jimbo la Mbogwe huku kwa upande wa wabunge wa viti maalumu walioteuliwa ni Regina Mikenze na Thabita Chagula.
Kikao cha Halmashuri Kuu ya CCM Taifa cha uteuzi wa wagombea hao wa nafasi za ubunge ,Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo na Viti Maalum kimeongozwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani jijini Dodoma.