Storm FM
Storm FM
23 August 2025, 8:14 pm

Malezi bora ndiyo msingi wa mafanikio ya baadaye kwani mtoto anayekuzwa katika mazingira mazuri huwa na nafasi kubwa ya kutimiza ndoto zake.
Na Mrisho Sadick:
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Sakika Mohamed amewataka wazazi na walezi kuweka kipaumbele katika malezi na makuzi ya mtoto badala ya kujikita zaidi kwenye shughuli za kiuchumi pekee.
Akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya shule ya msingi na awali ya Waja Spring Manispaa ya Geita Mkoani Geita leo Agosti 23,2025 Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwa malezi bora ndiyo msingi wa mafanikio ya baadaye kwani mtoto anayekuzwa katika mazingira mazuri huwa na nafasi kubwa ya kufanikisha ndoto zake.

Kwa upande wake Mkurugenzi mwenza wa shule za Waja, Jacqueline Tesha amesema shule hiyo imekuwa na historia ya kufanya vizuri kitaaluma tangu kuanzishwa kwake nakwamba mafanikio hayo yanatokana na mshikamanio wa walimu, wazazi na wanafunzi, huku akiwasihi wazazi kuendelea kushirikiana ili shule iendelee kushika nafasi ya juu kielimu nakuwataka wazazi na walezi kuweka nguvu katika malezi.

Awali muhitimu wa darasa la saba Grace Alex akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema wahitimu wa darasa la saba wako 85 , wavulana 40 na wasichana 45 nakwamba katika kipindi cha miaka saba wawapo shule wamekuwa na mafanikio makubwa hususani ya kitaaluma kwa kufanya vizuri katika mitihani ya ndani na nje ya shule hiyo huku akisisitiza malezi ndio msingi wa mafanikio kwa mtoto.