Storm FM

GGML yaridhia kuwalipa fidia wakazi Nyakabale na Nyamalembo

22 August 2025, 3:27 pm

Waziri wa madini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Nyakabale. Picha na Ester Mabula

Hatua hiyo imefikiwa baada ya pande zote kukubaliana kuanza mchakato wa ulipaji fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha maeneo yanayotumiwa na mgodi huo

Na: Ester Mabula

Serikali kupitia wizara ya madini imetangaza rasmi kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 26 kati ya Mgodi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani, hususani mitaa ya Nyakabale na Nyamalembo katika halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo waziri wa madini Mhe. Anthony Mavunde amesema GGML imeridhia kuanza mchakato wa fidia ambapo kuanzia Agosti 22, 2025 timu ya wataalamu wa serikali itaanza kazi ya uthamini wa mali kwa kipindi cha siku 40, ili kuhakikisha wakazi hao wanalipwa stahiki zao kwa wakati na kwa uwazi.

Sauti ya waziri wa madini Anthony Mavunde

Katika hatua nyingine ametahadharisha juu ya watu ambao watakwamisha zoezi hilo kwa kwenda kinyume ikiwemo kujenga kipindi ambacho tayari tathmini imekamilika.

Sauti ya waziri wa madini Anthony Mavunde
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela akizungumza na wananchi. Picha na Ester Mabula

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema mchakato wa utatuzi wa mgogoro huo haukuwa rahisi kwani mara kadhaa ulisababisha mvutano kati ya viongozi wa Serikali na uongozi wa GGML lakini hatimaye hatua ya maridhiano imefikiwa huku akiwapongeza wananchi kwa uvumilivu.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Geita

Wakazi wa Nyakabale na Nyamalembo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgodi wa GGML kwa jitihada kubwa za kuhakikisha mgogoro huo unafikia mwisho nakwamba hatua hiyo ni ushindi mkubwa baada ya miaka mingi ya changamoto na kusubiri kwa muda mrefu haki yao bila mafanikio.

Sauti ya wakazi wa Nyakabale na Nyamalembo
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nyakabale wakimsikiliza waziri wa madini. Picha na Ester Mabula