Storm FM
Storm FM
18 August 2025, 8:14 pm

Malengo mahususi ya mradi huo ni kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zitokanazo na Bomba la mafuta ghafi.
Na Mrisho Sadick:
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amezindua rasmi mradi wa kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwenye maeneo yaliyopitiwa na Bomba la mafuta Ghafi la Afrika Mashariki wilayani Bukombe Mkoani Geita unaotarajiwa kuwanufaisha vijana zaidi ya Elfu 12,000.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika uwanja wa Kijiji cha Bukombe wilayani Bukombe kwa awamu ya kwanza ambayo inahusisha mikoa ya Geita , Kagera,Tabora na Tanga wenye lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zitokanazo na Bomba la mafuta Ghafi huku Naibu Waziri Mkuu Dkt Doto Biteko amewataka wananchi waliopitiwa na mradi huo kuhakikisha wanaulinda kwakuwa umekuwa fursa kwao.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi ,vijana ,ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassa analipenda kundi la vijana ndio maana anaweka mazingira kwa kulipatia fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi huku Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akisema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa vijana wa Bukombe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Felchesmi Mlamba amesema Mradi huu wa Bomba la mafuta umefikia asilimia 65 ya utekelezaji wake nakwamba Katika mradi huu serikali ya Tanzania imewekeza kiasi cha shilingi Trilioni 1.12 huku meneja uwekezaji na uwajibikaji kwa jamii kutoka EACOP Clare Haule amesema mradi huo unakwenda kukabiliana na changamoto za ajira kwa kutoa ujuzi unaolingana na mahitaji ya soko.