Storm FM

Wajumbe wa CCM Mikononi mwa TAKUKURU Geita

14 August 2025, 4:17 pm

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita akizungumzia utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu. Picha na Mrisho Sadick

Wakati joto la uchaguzi Mkuu likiendelea kupanda TAKUKURU nayo imekaa mguu sawa kuhakikisha inakabiliana na vitendo vya Rushwa.

Na Mrisho Sadick – Geita

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita imewakamata nakuwahoji baadhi ya wajumbe wa UWT wilaya ya Geita Mkoani Geita baada ya kusambaa kwa picha mjongeo kwenye mitandao ya Kijamii ikionesha wanagawana pesa baada ya mchakato wa kuwanadi wagombea Ubunge kumalizika.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita James Ruge ametoa taarifa hiyo leo Agosti 14,2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake kuhusu taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kuanzia mwezi April hadi Juni ,2025 ambapo amesema tukio hilo limewahusisha wajumbe wa Kata ya Nyankumbu Manispaa ya Geita baada ya zoezi la kuwanadi wagombea Ubunge kumalizika.

Mkuu wa TAKUKURU Geita akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Ruge amesema katika tukio lingine TAKUKURU imewakamata nakuwahoji baadhi ya wajumbe wa CCM katika Jimbo la Chato kaskazini Kata ya Bukome Kijiji Cha Buzirayombo wilayani Chato baada ya kusambaa kwa picha mjongeo zikionesha tukio la kupikwa kwa chakula na vinywaji wakati wa zoezi la upigaji wa kura za maoni.

Sambamba na hayo TAKUKURU Geita imefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 770 kati ya 930 zilizokopwa katika Benki ya NBC na vyma vya msingi vya ushirika vya wakulima wa Tumbaku wilayani Mbogwe Mkoani Geita nakushindwa kuzirejeshwa.

Sauti ya Ripoti kamili ya stori hii