Storm FM

Wanawake na Samia zaidi ya 100 wanufaika na mafunzo ya VETA Geita

12 July 2025, 4:14 pm

Wanawake wanaonufaika na mafunzo ya VETA Geita wakiwa darasani. Picha na Kale Chongela

Baada ya serikali kuwasisitiza watanzania kuchangamkia fursa ya elimu ya ufundi wanawake Geita wamejitokeza katika chuo cha VETA kupatiwa mafunzo katika fani mbalimbali.

Na Kale Chongela:

Wanawake na Samia zaidi ya 100 wanaonufaika na mafunzo ya ufundi stadi kutoka Chuo cha VETA Manispaa ya Geita wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fursa ya mafunzo hayo bila malipo, wakisema yamewawezesha kupata ujuzi wa kujiajiri.

Wakiwa kwenye mafunzo hayo Katika Chuo hicho Cha VETA Manispaa ya Geita baadhi ya wanawake hao wamesema hatua hiyo ni mkombozi kwa wanawake wengi waliokuwa hawana nafasi ya kupata elimu ya ufundi kutokana na changamoto za kifedha.

Sauti ya Wanufaika wa Mafunzo

Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Geita Bi Adelina Kabakama, amewashauri wanawake hao kuhakikisha wanajisajili kwenye mfumo wa National Economic Support Tool (NEST) ili waweze kunufaika na tenda mbalimbali zinazotangazwa na serikali.

Wanawake wanaonufaika na mafunzo ya VETA Geita wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo cha VETA. Picha na Kale Chongela
Sauti ya katibu wa VETA Geita

Kwa mujibu wa uongozi wa Chuo cha VETA Manispaa ya Geita, jumla ya wanawake 112 wamejitokeza kuchangamkia mafunzo hayo ya muda mfupi katika fani tatu za Upishi, Ufundi Bomba, na Ufundi Umeme.

Wanawake wanaonufaika na mafunzo ya VETA Geita wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo cha VETA. Picha na Kale Chongela

Mkuu wa chuo hicho amesema hatua hii inaonesha namna wananchi wanavyoitikia wito wa serikali katika kukuza ujuzi wa kujitegemea, huku akiwakaribisha wananchi zaidi kujiunga na chuo hicho kupata mafunzo katika fani mbalimbali.

Saut ya Mkuu wa VETA Geita

Kwa sasa, VETA ina zaidi ya vyuo 50 nchini Tanzania, vikitoa mafunzo ya ufundi kwa maelfu ya vijana na watu wazima, kwa lengo la kukuza ajira na ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la sasa.